KAMATI YA BUNGE YA MAJI YAKAGUA MRADI WA MAJI WA ICS WILAYA YA KISHAPU | LUKAZA BLOG

KAMATI YA BUNGE YA MAJI YAKAGUA MRADI WA MAJI WA ICS WILAYA YA KISHAPU

Kufuatia maadhimisho ya wiki ya maji duaniani, serikali imeunga mkono na kulipongeza shirika la ICS kwa jitihada zake kubwa za kuhakikisha ...

Kufuatia maadhimisho ya wiki ya maji duaniani, serikali imeunga mkono na kulipongeza shirika la ICS kwa jitihada zake kubwa za kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wanapata maji safi yanaozalishwa kutoka katika ziwa Victoria. Kamati hiyo ya maji kutoka bungeni iliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Merry Nagu pamoja na wajumbe wake 30. Shirika la ICS limekwisha kamilisha mradi huo kwa asilimia 100% na lipo tayari kuanza kuwanufaisha wananchi wake kwa maji hayo.
 Kufuatia mradi huo kushirikiana bega kwa bega na serikali ya wilaya ya Kishapu, ICS inasubiri tamko la serikali ambalo linahusisha upangaji wa bei ya maji hayo kutoka EWURA. Akiwatoa wasiwasi wananchi pamoja na viongozi wa kamati ya bunge ya maji juu ya uwahishwaji wa bei hio kutoka EWURA, Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Kishapu bwana Lucas Said alisema zoezi hilo lipo katika hatua za mwisho na bei itatangwa hivi karibuni ili wananchi wanufaike na maji hayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba pamoja na mradi wa ICS kuwa tayari bado wananchi wanafata maji umbali mrefu na pia wananunua dumu moja kwa shilingi 500.

Kamati ya bunge ya maji liadhimia kwa pamoja kuwa kwa kuwa ICS wamekwisha kamilisha mradi kwa asilimia 100% na bei pendekezi kutoka kwa wananchi na wilaya ya kishapu kwenda EWURA ni shilingi 30 kwa kila ndoo kinachosubiriwa ni idhini au maboresho ya EWURA juu ya tamko hilo, Kamati ya bunge imewataka ICS kuanza kuuza maji kwa shilingi 30 mpaka pale EWURA watakapotoa tamko. Na kuonesha kuwa kamati hiyo iliazimia kuanza kuwa maji mananchi baadhi ya wanakamati walitoa kiasi cha fedha na kuwanunulia maji wananchi hivyo zoezi hilo likaanza. 
 Kufuatia teknolojia itakayotumika katika ununuaji wa maji hayo kuwa mpya kabisa machonii mwa wanakishapu, Bi Lucy Charles, mhandisi msaidizi wa Shirika la ICS aliwatoa wasiwasi kwa kuwaeleza kuwa wananchi watapewa mafunzo ya kutosha ambayo tayari yameshaanza kutolewa ili kila mwananchi apate maji kwa wakati na bila usumbufu. Maji hayo yatanunuliwa kuwa mfumo wa Malipo ya Kabla, ambapo kila mwananchi atapewa kadi yake bure, ili kuweka salio katika kadi hiyo anatakiwa kwenda kwa wakala wa maji ambapo mawakala hao wanapatikana katika maduka ya kawaida ya bidhaa za nyumbani. Mwananchi ataweka vocha ya maji kulingana na pesa aliyonayo na pia ataninunua kulingana na haja yake na salio kama ni kubwa zaidi ya kiasi anachota basi pesa yake itaendelea kutunzwa katika kadi yake na atakatwa aliyotumia.
 Shirika la ICS lenye lengo la kuhakikisha mtoto na mwanamke wanakuwa katika mazingira salama yatakayoifanya jamii iishi katika familia zilizo na afya salama, limetumia milioni  mia saba hamsini na tano (Tsh 755,000,000) kujenga mradi wa maji katika vijiji vya Maganzo na Masagala wilayani Kishapu. Shirika hilo limeyatekeleza hao kwa udhamini mkubwa wa HDIF na UK Aid.

Related

Hot Stories 7795192798760330097

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item