NAY WA MITEGO AACHIWA HURU | LUKAZA BLOG

NAY WA MITEGO AACHIWA HURU

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kushikiliwa na maafisa wa...

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kushikiliwa na maafisa wa polisi nchini, kuhusiana na wimbo wake wenye jina la "Wapo", ameachiliwa huru mchana wa leo.

Nay wa Mitego ameachiliwa huru kufuatia uamuzi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kupokea ushauri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 

Hata hivyo Waziri Mwakyembe alimtaka Nay wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake.

Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.

Related

Hot Stories 6890415217779020372

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item