Ruge Afunguka Kuhusu Clouds kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa | LUKAZA BLOG

Ruge Afunguka Kuhusu Clouds kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa

Mkurugenzi wa Vipindi na Uendeshaji wa Kituo cha Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefunguka Jumatatu hii katika kipindi Clouds 360 cha ...

Mkurugenzi wa Vipindi na Uendeshaji wa Kituo cha Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefunguka Jumatatu hii katika kipindi Clouds 360 cha Clouds TV na kuthibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho.

Hayo yametokea baada ya weekend hii kupitia mitandao ya kijamii kusambaa video inamonyesha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiingia ofisi za Clouds usiku akiwa na askari ambao wana burunduki.
Ruge aliyekuwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast, Masoud Kipanya alisema alipigiwa simu na mmoja wa wafanyakazi wake kuwa Makonda ameingia ofisini hapo akiwa na polisi wenye silaha.
“Jambo hili limeniumiza sana, kwani pamoja na kuwa Makonda ni rafiki yetu lakini hatukutegemea kama angeweza kuingia ofisini na polisi wenye silaha,” alisema na kuongeza
“Hata kama ni rafiki yako, siku moja akiingia nyumbani kwako usiku sana na silaha lazima uhoji.” aliongeza Ruge.

Related

Hot Stories 4798022623113460524

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item