Skuli ya Kijini na Mbuyu Tendee Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,Wafaidika na Mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Cha PennyRoyal kwa Kutoa Elimu ya Afya na Mazingira | LUKAZA BLOG

Skuli ya Kijini na Mbuyu Tendee Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,Wafaidika na Mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Cha PennyRoyal kwa Kutoa Elimu ya Afya na Mazingira

Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA anayetowa mafunzo ya Afya na maz...

Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA anayetowa mafunzo ya Afya na mazingira kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijini Matemwe akizungumza na waandishi wa habari kufanikiwa kwa zoezi hilo la kutowa elimu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo jinsi ya kuhifadhi mazingira na afya yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Kitalii Matemwe Pennyroyal kwa kutowa elimu hiyo.
Amesema umeleta mafanikio makubwa kwa watoto hao jinsi ya kujilinda na maradhi ya mripuko kwa kupata elimu hiyo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa SUZA Nahya Khamis Nossor akitowa mafunzo ya Afya ya Mazingira kwa Wanafunzo wa Skuli hya Sekondari ya Kijini Matemwe jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko kwa kutunza mazingira safi katika maeneo yao na skuli, Mradi huo wa Elimu hiyo unafadhiliwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe  Pennyroyal.  
Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatila mafunzo hayo wakiwa katika darasa wakifuatilia kwa utulivu  wakiangalia vipeperushi vinavyoelezea utungaji wa Afya na Mazingira katika jamii.


Afisa Afya na Mazingira Bi Zeldat Masoud Khamis akitowa mafunzo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe jinsi ya elimu ya afya ya mazingira kwa wanafunzi hao. 
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia Mafunzo hayo yanayotolewa na Maafisa wa Afya na Mazingira wakitowa elimu hiyo.
Wankatika mafunzo ya vitendo jinsi ya kusafisha mikono kujinginga na maradhi na kuweka mazingira mazuri ya afya yake. kwa kutumia maji na sabuni kufanya usafi kabla ya kula na baada ya kutoka msalani.


Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe wakifuatilia kipeperushi kinachoelezea Afya ya Mazingira. wakati wa mafunzo yao. 
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatila vipeperushi vinavyoeleza utunzaji wa Afya na Mazingira ili kujikinga na maradhi ya matumbo na kipindupindu, Mafunzo hayo yanatolewa na Mradi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara. Blogspot.com
Zanzinews.com
email.othmanmaulid@gmail.com. 

Related

kitaifa 120854813986154376

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item