TDL Imesitisha utengenezaji pombe kwa vifungashio vya plastiki | LUKAZA BLOG

TDL Imesitisha utengenezaji pombe kwa vifungashio vya plastiki

Mfano wa chupa za kisasa zitakazotumika kufungashia bidhaa za TDL  -Serikali yakuta hakuna uzalishaji wowote unaendelea Kam...

Mfano wa chupa za kisasa zitakazotumika kufungashia bidhaa za TDL 
-Serikali yakuta hakuna uzalishaji wowote unaendelea
Kampuni ya TDL maarufu konyagi imesitisha utengenezaji za pombe kwa kutumia vifungashio vya plastiki kwa mujibu wa agizo la serikali ambapo mwisho wa kusambaza pombe hizo ulikuwa jana.
Maofisa kutoka Mamlaka ya kusimamia vyakula na Madawa (TFDA),NEMC,TBS na Jeshi la Polisi wamefika kiwandani leo na kukuta hakuna uzalishaji wa vinywaji hivyo unaoendelea kama ambavyo kuna taarifa za kupotosha kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa TDL imekaidi agizo la serikali na imekutwa ikiendelea kufanya uzalishaji kwa kutumia vifungashio vilivyoipigwa marufuku na serikali.

TDL siku zote imekuwa ikiendesha shughuli zake za kibiashara kwa kufuata miongozo na sheria za serikali kupitia taasisi mbalimbali hiyo haiwezi kukaidi na kuendelea na uzalishaji wa kutumia vifungashio vya plastiki wakati vimepigwa marufuku bali inajipanga kutumia teknolojia za kutumia vifungashio vilivyotengenezwa kwa malighafi ya kioo ambavyo vina ubora  wa hali ya juu na salama kwa kuwa sio rahisi kuviigiza.

Related

Biashara 1740061975000254665

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item