MISS TANZANIA DIANA EDWARD AKAMILISHIWA ZAWADI ZAKE | LUKAZA BLOG

MISS TANZANIA DIANA EDWARD AKAMILISHIWA ZAWADI ZAKE

 Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa (kulia) akimkabidhi fedha taslim kiasi cha Sh. Milioni mbili (2Mil.), Mrembo mw...


 Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa (kulia) akimkabidhi fedha taslim kiasi cha Sh. Milioni mbili (2Mil.), Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward ikiwa ni sehemu ya stahiki yake aliyotakiwa kuipata baada ya kutwaa taji hilo, mapema mwaka jana. Fedha hizo zimetolewa na Mmoja wa Wadhamini wa shindano hilo, ambao ni Duka Maarufu kwa Uuzaji wa vito vya thamani la Gift Jewellers lililo ndani ya Jengo la City Mall, Jijini Dar es salaam. Kamati ya Miss Tanzania mwezi jana iliahidi mbele ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa ingeweza kumalizana na Mrembo huyo mapema mwezi huu na sasa wamekamilisha deni hilo kupitia kwa Mdhamini wao ambaye ni Gift Jewellers. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Aprili 7, 2017. Kulia ni Meneja Masoko wa Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers, Faudhia Abdulrahman.

Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Masoko wa Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers, Faudhia Abdulrahman (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kumkamilishia fedha za zawadi zake kiasi cha shilingi Milioni 2 alizokuwa akidai Mrembo huyo kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya kushinda taji hilo mapema mwaka jana. Fedha hizo zimetolewa na Mmoja wa Wadhamini wa shindano hilo, ambao ni Duka Maarufu kwa Uuzaji wa vito vya thamani la Gift Jewellers lililo ndani ya Jengo la City Mall, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward akionyesha sehemu ya zawadi yake aliyopewa kutoka Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers muda mfupi baada ya kukabidhiwa kitita chake. Wengine pichani toka kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa, Meneja Masoko wa Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers, Faudhia Abdulrahman pamoja na Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa Miss Tanzania, Albert Makoye.
 
 Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward akipozi kwa picha nje ya Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers.

Related

Hot Stories 3855948230232872475

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item