MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA | LUKAZA BLOG

MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA

Na Leonce Zimbandu MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha shukrani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani k...

Na Leonce Zimbandu


MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha shukrani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani kata ya Majohe, Gabriel Macheho (pichani) baada ya kutambua mchango wake wakuhifadhi na kutunza rasilimali za umma. 


Moja ya rasilimali hizo ni pamoja na kusimamia eneo la umma lisichukuliwe na kumilikiwa na watubinafsi, likiwamo eneo  la machimbo ya mchanga lililokuwa likimilikiwa na Mbezi Tile. Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu alimkabidhi Macheho cheti hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi ili kutoa motisha kwa wananchi wenye moyo wakutoa utetezi wa mali za umma.

Alisema  Manispaa imeamua kutoa cheti hicho baada ya kutambua mchango aliotoa mkazi huyo kwa kufuatilia hadi kufanikiwa kupatikana kwa eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii, ikiwamo ujenzi wa soko na shule. “ Tunapaswa kuonesha uzalendo wakufuatilia mambo yenye manufaa kwa jamii ilikuishaidia jamii inayo kuzunguka,” alisema.

Mkazi wa Majohe Andrew Msuya alisema amefurahishwa na kitendo cha Serikali kutambua mchango wa wananchiwachini,  hiyo italeta chachu kwa watu wengine kuendeleza na kuhifadhi mazingira.
Naombaserikalikuendeleakuthaminimchangowawatuwachinikwakutoamotishailikukuzauhusianomzuri,”alisema.

Gabriel Macheho ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wake wa kutunza na kuhifadhi rasilimali za umma, kwani wananchi wengi hawakujua kama huo ulikuwa ni wajibu wa msingi kutekeleza.

“Nitaendelea kutoa mchango wangu kwa serikali na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha maeneo ya umma yanaendelea kulindwa na kuhifadhiwa,”

alisema.

Related

kitaifa 2375279135121187807

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item