Mshindi wa Mwanza atua Dar kubeba mamilioni yake | LUKAZA BLOG

Mshindi wa Mwanza atua Dar kubeba mamilioni yake

Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko Tanzania kutoka jijini Mwanza Pildas Emmanuel kushoto akipeana mikono ya shukrani na Meneja Masoko wa B...


Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko Tanzania kutoka jijini Mwanza Pildas Emmanuel kushoto akipeana mikono ya shukrani na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven baada ya kumkabidhi fedha zake jijini Dar es Salaam kama sehemu ya ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko inayoendelea nchini Tanzania na kugawa mamilioni kwa washindi wake.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la mchezo bahati na nasibu la Biko Ijue Nguvu ya Buku, limemkabidhi mshindi wake wa wiki ya tatu ya Sh Milioni 10, ambaye ni Pildas Emmanuel, anayeishi jijini Mwanza baada ya kutangazwa mshindi wa wiki katika droo iliyochezeshwa Jumapili iliyopita.

Makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam sambamba na kumfungulia akaunti ya benki ya NMB kwa ajili ya kuingiza fedha hizo kwa mshindi huyo aliyejitambulisha kama mjasiriamali wa vileo jijini Mwanza
Tanzania.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumpa elimu ya kifedha mshindi huyo, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema sasa Biko limekolea na wameendelea kumwaga fedha kwa kila mshindi wao, akiwamo Emmanuel aliyeletwa kwa Ndege kwa ajili ya kumkabidhi fedha zake.

Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kulia, akishuhudia jinsi mshindi wao wa Sh Milioni wa bahati nasibu ya Biko, Pildas Emmanuel anavyofurahia baada ya kumkabidhi fedha zake mapema wiki hii jijini Dar es Salaam. Na Mpiga Picha wetu.


Alisema kila siku wamekuwa wakilipa zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh 1,000,000, pamoja na
zawadi kubwa ya wiki ya Sh Milioni 10 kwa kila mshindi wao, huku wakiwa
wameshalipa kiasi hicho kwa washindi wawili ambao ni Christopher Mgaya, Nicholaus Mlasu ambao wote wameshapokea fedha zao.

“Biko limekolea na linaendelea kuwapatia utajiri wananchi wa Watanzania
wanaothubutu kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo,
Vodacom na Airtel, ambao ni mchezo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwa
kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumalizia namba ya
kumbukumbu ambayo ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa sh 1000.
“Na kila Sh 1000 itakayolipwa itakuwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku mshiriki akiruhusiwa kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko ili wavune mamilioni ya Biko.

Naye Emmanuel alisema kwamba amefurahishwa na huduma zote alizopewa na Biko ikiwamo ya kumpa fedha zake katika benki ya NMB pamoja na kumleta jijini Dar es Salaam kwa ndege kutoka Mwanza jambo ambalo halijawahi kumtokea katika maisha yake.

“Ingawa nimepata fedha nyingi ambazo sijawahi kuzishika tangu nizaliwe, pia nimeingia kwenye historia kwa sababu na mimi nimepanda ndege kwa mara kwanza huku fedha zote zikilipwa na Biko, hivyo ni kampuni nzuri na
mchezo wao ni mzuri kutokana na malipo ya ushindi kulipwa haraka,” Alisema Emmanuel na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.

Emmanuel aliwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu akitokea jijini Mwanza ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja katika droo iliyoshuhudiwa pia na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Related

Biashara 1513755117139347586

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item