TBL Group yaadhimisha Wiki ya Usalama sehemu ya kazi kwa vitendo | LUKAZA BLOG

TBL Group yaadhimisha Wiki ya Usalama sehemu ya kazi kwa vitendo

Wafanyakazi wapatiwa mafunzo ya usalama Kampuni ya TBL Group imeweka mikakati kuhakikisha viwanda vyake vyote nchini vinatekeleza kanuni ...

Wafanyakazi wapatiwa mafunzo ya usalama
Kampuni ya TBL Group imeweka mikakati kuhakikisha viwanda vyake vyote nchini vinatekeleza kanuni za Afya na Usalama mahali pa kazi na nje ya kazi kwa viwango vya kimataifa.

Akiongea wakati wa kilele cha wiki ya Usalama mahali pa kazi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni iliandaa mafunzo mbalimbali ya Usalama kwa wafanyakazi wake na kushiriki maounyesho ya usalama mahali pa kazi yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro,Meneja wa Usalama na Afya kwa TBL,Renatus Nyanda,alisema kuwa usalama sehemu za kazi ni moja ya suala ambalo kampuni inalipa kipaumbele kikuu na kuhakikisha  hakujitokezi matukio ya ajali maeneo ya kazi.

Usalama ni suala tunalolipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa bila kuwepo usalama sehemu za kazi ni vigumu kufanya kazi kwa ufanisi na ndio maana tunashikilia rekodi ya kushinda tuzo ya Usalama Mahali pa Kazi inayotolewa na taasisi ya Tanzania Occupational Health and Safety Agency  (OSHA) na tuzo ya shirikisho la kimataifa la kusimamia masuala ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini Afrika ya Kusini  lijulikanalo kama National Occupational Safety Association (NOSA)”
Alisema kampuni kutokana na  suala la usalama kupewa kipaumbele matukio ya ajali yamekuwa yakipungua mwaka hadi mwaka katika shughuli za uzalishaji viwandani kwa kuwa kila mfanyakazi amefundisha kulinda usalama wa kwake binafsi na wenzake na usalama huo umekuwa hauishii kwa wafanyakazi tu bali na wakandarasi na wageni wanaotembelea maeneo ya kampuni usalama wao unazingatiwa.

Aliwapongeza wafanyakazi wote kwa jinsi wanavyoshiriki kuzingatia kanuni na miongozo inayowekwa na kampuni ikiwemo kufunga mashine za kisasa hali  ambayo inachangia kuleta mafanikio na kuvifanya viwanda vilivyopo chini ya TBL Group kuongoza kufanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa na viwanda vingine  nchini

Katika maadhimisho ya Wiki ya Usalama Kazini iliyofikia kilele mwishoni mwa wiki wafanyakazi wote wa kampuni ya TBL Group walihudhuria semina mbalimbali za ndani zilizoendeshwa na wataalamu kutoka taasisis mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kuhusiana na masuala ya usalama mahali pa kazi.Viwanda vya kampuni ya TBL Group hapa nchini vipo katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza.
 Wafanyakazi wa Chibuku wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya Usalama mahali pa kazi
 wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Ilala wakifuatilia mada za usalama
 Wafanyakazi wa Konyagi wakipigwa msasa kuhususiana na usalama mahali pa kazi
 
 Waziri wa  Sera,Bunge,Vijana,Ajira na Walemavu,Jenista Mhagama, (Kushoto) akipata maelezo ya kanuni za usalama za kampuni wa TBL Group  kutoka kwa Meneja Usalama wa TBL Group (TBL Safety Manager),Renatus Nyanda,wakati alipotembelea banda ya maonyesho ya Wiki ya Usalama mahali pa kazi yaliyomalizika  katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki
 Wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Mwanza wakifuatilia mada za usalama
Wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Arusha wakipigwa msasa wa masuala ya usalama

Related

Hot Stories 190877277828929411

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item