Trust Care Tanzania Foundation yawanoa wanafunzi vyuo vikuu Dar | LUKAZA BLOG

Trust Care Tanzania Foundation yawanoa wanafunzi vyuo vikuu Dar

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Dk. Rodrick Ndomba akizungumza kufungia semina ya wanavyuo iliyoa...Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Dk. Rodrick Ndomba akizungumza kufungia semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) na kushirikisha wanafunzi anuai kutoka vyuo vya IFM, CBE, DIT, DUCE, TIA, UDSM, MUHAS, CHUO CHA DIPLOMASIA, KIU, CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI.

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation.

Msanii Nick Wa Pili akiwasilisha mada leo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

MKURUGENZI Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo. Alisema mada zilizotolewa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo, Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo.
Kwa upande wa wadhamini wakuu wa semina hiyo Kampuni ya TTCL, Injinia Enocent Msasi Mkurugenzi wa Biashara TTCL alisema kampuni hiyo imeunga mkono kampuni ya Trust Care Tanzania kwa dhumuni lake la kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta za kiafya, kielimu na kijamii. Aliongeza kuwa lengo hilo linashabihiana na lengo la TTCL kuhakikisha inakuwa na jamii bora zaidi kiteknolojia, kielimu, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla.
“TTCL imedhamini semina hii kwasababu inatoa mchango mkubwa katika kujenga taifa lenye vijana wachapakazi, vijana wenye mtizamo chanya, vijana wenye uwezo wa uthubutu, na kupambana na changamoto mbalimbali za kimaisha, ” alisema Msasi na kuongeza kuwa TTCL kupitia huduma zake bora za intaneti, sauti na SMS inawaunga mkono vijana mara zote na itakuwa mstari wa mbele kufanikisha juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation.
Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Mmoja wa wawasilishaji mada kwa wanafunzi (hawapo pichani) wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).
Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) nje ya ukumbi wa semina hiyo leo.
Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Related

kitaifa 9196210818940084748

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item