Ufinyu wa bajeti ni kikwazo kwa huduma za Uzazi wa Mpango | LUKAZA BLOG

Ufinyu wa bajeti ni kikwazo kwa huduma za Uzazi wa Mpango

 Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango imekuwa ndicho kikwazo kikuu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hapa nch...

 Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango imekuwa ndicho kikwazo kikuu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hapa nchini ambapo  katika miaka sita iliyopita kiwango cha juu sana kilichotengwa na
kutolewa kwa mwaka ni shilingi bilioni tano tu.

Hayo yameelezwa  na Dkt. Faustine Ndugulile, ambaye ni Mjumbe wa Chama cha Wabunge kuhusu Idadi ya Watu na Maendeleo mwishoni mwa wiki wakati akiongea jijini Dar es Salaam kuhusu changamoto cha uzazi wa mpango hapa nchini Tanzania.

Dkt Ndugulile alisema kuwa huduma za uzazi wa mpango zinahitaji shilingi bilioni 20 kila mwaka lakini kati ya mwaka 2010/11 na 2015/16 ni bilioni 5 tu zilizotengwa na kutolewa kila mwaka zilikuwa pungufu sana  ukilinganisha na mahitaji halisi. Kiwango cha juu kwa mwaka kilikuwa ni  kiasi cha shilingi bilioni tano tu ambazo zilitengwa na kutolewa, sawa  na asilimia 25 tu ya mahitaji yote kwa mwaka husika.

‘Tafiti  zinaonyesha kuwa Tanzania ni moja kati nchi zenye vifo vingi vitokanao  na uzazi duniani, ambapo vifo 556 hutokea kwa kila vizazi hai 100,000;  ikimaanisha kuwa zaidi ya akinamama 50 hufariki kila siku kutokana na  matatizo ya uzazi’, alisema Ndungulile.

Dkt Ndugulile aliongeza  kuwa zaidi ya watoto 100,000 hufariki kabla ya kutimiza miaka mitano,  kati ya hao zaidi ya 50,000 hufariki kabla ya kuzaliwa na nusu yao  wakati wa kuzaliwa, huku wenzao wapatao 40,000 wakifariki dunia kwenye  siku 28 za mwanzo baada ya kuzaliwa. Licha ya ufinyu wa bajeti, Vifo  vingi vya uzazi hutokea kwa sababu wanawake wanakosa kufikia huduma  ambazo wanazihitaji ikiwemo uzazi wa mpango.

Sababu zingine ni  kubeba mimba wakati wa umri mdogo, kutoa mimba kwa njia zisizo salama,  kuendelea kubeba mimba wakiwa na umri mkubwa ambao ni zaidi ya miaka 35, na kukosa ufahamu wa jinsi ya kutoa nafasi baada ya kujingua ili kubeba mimba inayofuata.

Mpango wa Taifa Uliokasimiwa wa Uzazi wa  Mpango (NFPCIP) uliweka lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi  kupitia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango hadi kufikia asilimia 60 ya wanawake walio katika umri wa uzazi ilipofika mwaka 2015. Ni asilimia  32 tu ya wanawake walifikiwa. Lengo hilo limehishwa kwa ajili ya  kufikiwa mwaka 2020.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa za uzazi hapa  nchini, Dr. Faustine Ndungulile alisema kuwa “ufinyu wa bajeti umekuwa  ikiwanyima wanawake wenye umri mdogo huduma za uzazi wa mpango ambazo ni
muhimu kwa afya zao, watoto wao, na maendeleo yao na taifa. Wanawake  wanaoanza uzazi katika umri mdogo na kuzaa kwa mfululizo wanakosa fursa  za kujiendeleza kielimu, kiuchumi, na kijamii; na kuwafanya wasiweze
kufikia upeo wa ndoto zao za kimaendeleo, hali ambayo pia huwapata  watoto wao.”

Related

Afya 4290151930723692445

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item