Hivi ndivyo Watanzania walivyotoa heshima za mwisho kwa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Marehemu Ndesamburo | LUKAZA BLOG

Hivi ndivyo Watanzania walivyotoa heshima za mwisho kwa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Marehemu Ndesamburo

Viongozi wa juu wa Chadema, Freeman Mbowe na Edward Lowassa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, Phillemon Nd...

Viongozi wa juu wa Chadema, Freeman Mbowe na Edward Lowassa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo.

Ndesamburo alifariki ghafla wiki iliyopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mwili wa Ndesamburo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi Mjinim,utaagwa katika viwanja hivyo na leo saa kumi jioni utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga Ndesamburo.
  Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo lilielekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye uwanja  huo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili atika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo. 
Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na dini wakiwa wamesimama mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo kuwasili uwanjani hapo


 Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye uzuni mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ulipokuwa unaelekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo. 
  

Related

Siasa 8173714467713904526

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item