MAGARI 40 YANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) KANDA YA KATI, WA KUBAINI VYOMBO VYA MOTO VYENYE BIMA FEKI. | LUKAZA BLOG

MAGARI 40 YANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) KANDA YA KATI, WA KUBAINI VYOMBO VYA MOTO VYENYE BIMA FEKI.

Meneja  wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini  Kanda ya Kati  Bi.Stella Rutaguza akizungumza na madereva pamoja na  makondakta katika st...

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini  Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza akizungumza na madereva pamoja na makondakta katika stendi kuu ya mabasi mkoani Tabora ,walipokwenda kugagua bima za vyombo vya moto kama ni halali ama feki.Picha na Vero Ignatus Blog
 
Afisa Mwandamizi wa Bima Maneno Adam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima( TIRA)akikagua gari ili kuangalia kama bima inayotumika kama ni halali ama ni feki 

  Ukaguzi wa magari ukiendelea katika stendi kuu ya  mabasi Mkoani Tabora kama inavyoonekana kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda ya kati kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini   bi.Stella Rutaguza akiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani  Koplo Clement   .Picha na Vero Ignatus Blog.
Zoezi  la ukaguzi likiendelea wakati huohuo madereva ,makondakta pamoja na abiria wakipata elimu namna ya kutambua Bima kama ni halali ama  feki.Picha na Vero Ignatus Blog.
 
Wananchi ,madereva ,makondakta wa mabasi makubwa na madogo wakipewa elimu na namna ya kut5ambua bima feki kwa kutumia  simu ya mkononi au kwa njia ya mtandao mfumo wa TIRA MIS .Picha na Vero Ignatus Blog.

 Na Vero Ignatus, Tabora

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imefanya zoezi la ukaguzi wa bima za vyombo vya moto katika manispaaa ya Tabora katika stendi kuu ya mabasi na kubaini magari mengi hayana bima na mengine yana bima tofauti na kile kilichoorodheshwa katika bima hizo.

Akizungumza juu ya zoezi hilo meneja ( TIRA) Kanda ya Kati Stella Rutaguza amesema kuwa katika wameweza kukagua magari zaidi ya 266 magari 27 yamebainika kuwa na bima za kughushi ,magari 13 hayakuwa na bima,magari mengine yanatumia bima za pikipiki,na baadhi ya magari madogo yanatumia bima za magari ya mizigo.

"Magari tuliyoyakagua na kuyakuta yana bima feki tumeyakamata na kuyapeleka kituoni ili kwamba watupe maelezo  kuwa hizo bima wamezipata wapi,"alisema

Amesema kwa ada za malipo ya bima kwa mujibu wa sheria kwa maana ya bima ndogo (Third party insurance) kwa jumla magari haya 40 ni shilingi Milioni  33,850,000/= ambapo magari hayo yaliyokamatwa ni mabasi ya abiria 65,Coster za abiria 26, Noa na magari madogo ya binafsi.

 Imebainika kuwa kuna wamiliki wa magari ambao  walikuwa wamenunua bima kubwa (Comprehensive Insurance) ambapo kwa mabasi walikuwa wamelipia kuanzia shs.3,000,000/= na zaidi ambazo zimeingia kwenye mifuko ya matapeli wa bima.

"Tunataka hawa vishoka wa bima feki watafute kazi nyingine  halali za kufanya  kwani Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini haitawafumbia macho wadanyanyifu hawa

Bi Stella  amesema kuwa kesi za matapeli wa bima zimekuwa zikikaa muda mrefu bila kupekekwa mahakamani na hata zikipelekwa zimekuwa zikichukua  pia muda mrefu pia.

'Tunaomba kesi za Bima ziwe zinashughulikiwa kwa haraka na mamlaka husika "alisisitiza bi Stella. 

Meneja huyo wa kanda ya kati Stella ametoa  rai kwa mawakala wa bima na kusema kuwa yeyote atakayegunduliwa anauza  bima feki atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria na   atafutiwa leseni  maana amekiuka taratibu za kisheria

" Hawa watu wengi wanaouza hizo feki bima siyo wakala wa bima ila ni matepeli  tu wamtaani hivyo tukiwabaini tutawapeleka kwenye vyombo vya sheria hatuna utani wala mchezo katika hili".alisema.

Namna ya KUHAKIKI BIMA Kama ni  HALALI ama feki 

Kwa njia  ya simu ya mkononi  nenda kwenye uwanja wa ujumbe  mfupi  andika neno STIKA weka namba ya stika tuma  kwenda namba 15200

Kwa  kupitia njia ya mtandaoni (internet)kwenda kwenye tovuti ya Tira

mis  http/mis.tira.go.tz kisha ingiza namba za stika na bofya hakiki.

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item