MAKAMU WA RAIS,SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES | LUKAZA BLOG

MAKAMU WA RAIS,SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES

Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan b...

Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo. 

Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Abraham Ntambara.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama 
cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa 
ajili ya maisha yao ya baadaye.


Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati 
akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete 
anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12. 
“Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais.


Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza 
majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa
kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu 
mengine.


Aliahidi kuifanyia changamoto iliyotajwa ya matumizi ya 
mitandao ya kijamii ambapo alisema atalisimamia hilo kwani ni vizuri kutumia
mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili kutokana na hivi sasa watu kuitumia
vibaya. Pia alitoa pendekezo la chama hicho kubuni miradi mingine
ambayo inaweza kuwaingizia fedha ili kuacha kutegemea wahisani.


Mama Salma Kikwete wakati akimuachia jukumu hilo la kukilea 
chama hicho alimkabidhi vitu vitatu ambavyo ni Bendera ya Taifa ya chama, 
Katiba na mpango mkakati wa chama na kumvalisha Skafu ya chama kama ishara ya 
kukabidhiwa rasmi kijiti hicho.


Aidha alisema kuwa chama kimekuwa na mafanikio makubwa ikiwa 
ni pamoja na kuweza kuongeza wanachama kutoka 97,143 hadi kufikia wanachama 100,008 
mwaka huu.


Aliongeza kwamba wanatarajia mwezi Septemba kuapisha 
wanachama 300 katika mkoa huku akieleza kwamba tayari wamekwisha sajili zaidi 
ya wanachama 2000 katika mkoa wa lindi.
Kikundi cha sanaa cha Ilala kikitumbuiza 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye pia ni Kamishna wa TGGA, Sophia Mjema akimlaki aliyekuwa Mlezi wa TGGA Mama Salma Kikwete
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA
Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides
Samia akipata maelezo  kutoka kwa Mkufunzi wa Girl Guides Ruth kuhusu kazi mbalimbali za TGGA
Samia na Salma Kikwete wakilakiwa na Girl Guides
Brass Band ya Polisi ikiongoza wimbo wa Taifa
Viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo
Baadhi ya makamishna wa TGGA wakiwa katika sherehe hiyo
Mwenyekiti wa TGGA Profesa Martha Qorro akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa
Kamishna Mkuu wa TGGA Symphorosa Hangi akisema neno la utangulizi pamoja na kutambulisha  wageni waalikwa 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Abdalah akihutubia wakati wa sherehe hiyo
Aliyekuwa Mlezi wa TGGA, Mama Salma Kikwete akihutubia kabla ya kumkabidhi ulezi Makamu wa Rais Samia
Ni furaha iliyoje
Salma Kikwete akimvisha skavu Mlezi mpya wa TGGA, Samia Suluhu Hassan
Wasanii wa Shule ya Msingi Umoja wakitumbuiza wakati wa sherehe hiyo
Ni wakati wa furaha
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema na Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdalah wakichenza ngoma

Mama Samia akimtunza fedha kiongozi wa kikundi cha Umoja kwa kucheza vizuri
Kamishna Mkuu wa TGGA akimkabidhi zawadi ya saa  Mlezi mstaafu wa TGGA, Mama Salma Kikwete
Mama Salma akionesha Saa hiyo
Girl Guides wakighani shairi maalumu
Baadhi ya makamishna wakiimba wimbo maalumu
NI FURAHA TELE
Viongozi na makamishna wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi mpya wa TGGA, Samia

Mlezi mpya, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na makamishna wa mikoa

Mama Samia na Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA

Girl Guides wakiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Mlezi mpya, Samia


Related

kitaifa 8994248219967879067

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item