Hot News:Mahakama yatengua Uchaguzi wa Urais Kenya, Kurudiwa Ndani ya Siku 60 | LUKAZA BLOG

Hot News:Mahakama yatengua Uchaguzi wa Urais Kenya, Kurudiwa Ndani ya Siku 60

MAHAKAMA ya Juu nchini Kenya (Supreme Court), imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Laira Od...
MAHAKAMA ya Juu nchini Kenya (Supreme Court), imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Laira Odinga, na kuamuriwa kurudiwa kwa uchaguzi huo ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017.

Mahakama ya Juu nchini humo, imefikia uamuzi huo leo Septemba 1, 2017, kufuatia maombi ya Mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake, Bw. Raila Odinga, ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, uliompa ushindi Rais Kenyatta.

Katika maombi yake, Bw. Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matoko.

Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.Related

Hot Stories 1940211141758500399

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item