SBL yazindua bia mpya ya Plisner King | LUKAZA BLOG

SBL yazindua bia mpya ya Plisner King

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) Mjumbe  wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma(kushoto) na  Mkurug...

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) Mjumbe  wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma(kushoto) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka, wakigonga chupa za kinywaji kipya cha Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza mapema usiku wa jana .

Mhudumu akiweka chupa ya Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza juzi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(katikati)akiwa amevaa vazi la mfalme baada ya kuzindua bia mpya ya Pilsner King jijini Mwanza juzi, Mjumbe wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma kulia) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(katikati)akiwa amevaa vazi la mfalme baada ya kuzindua bia mpya ya Pilsner King jijini Mwanza juzi, Mjumbe wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma kulia) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) Mjumbea wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Chacha Gachuma(kushoto) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka, wakionja kinywaji kipya cha Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza mapema jana usiku.


Muonekano wa Chupa 

Wagon waalikwa wakiwa wanafuatilia shughuli za uzinduzi
Muda wa kuonja ladha ya Pilsner King mara baada ya uzinduzi mapema jana usiku katika Hotel 

Wagon waalikwa wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa pilsner king 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa katika picha ya pamoja na mwageni waalikwa mara baada ya   uzinduzi wa pilsner king mapema jana usiku Jijini Mwanza.


Mwanza, Septemba 20, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua bia mpya 

inayojulikana kama Pilsner King ambayo ni mwendelezo wa bia ya Pilsner Lager iliyozoeleka 
na ambayo ipo sokoni kwa kipindi kirefu.


Akizungumza 
wakati wa uzinduzi wa bia hiyo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL 
Cesear Mloka aliielezea bia hiyo mpya kama bia imara ambayo itakuwa kipenzi cha 
wanaume jasiri na wanaojiamini.


Bia ya Pilsner 
King ina kilevi cha asilimia 7.6%, na ndiyo bia imara kuliko zote 
zinazozalishwa hapa nchini.


Mkurugenzi 
huyo alifafanua kuwa, Pilsner King imetengenezwa na mzalishaji bia wa 
Kitanzania kwa kanuni za kimataifa akitumia malighafi za hapa nchini zenye 
ubora wa hali ya juu ambazo zimeipa bia hiyo ladha murua. “Hii ni kama zawadi 
kwa wanaume wa kweli baada ya shughuli nyingi za mchana kutwa,” anasema Mloka


Kwa mujibu wa 
mkurugenzi huyo, bia ya Pilsner imepata jina lake kutoka katika mji wa Pilsen 
uliopo Jamuhuri ya Czech ambako bia hiyo ilitengenezwa kwa mara ya kwanza na 
kuongeza kuwa, bia hiyo ya kipekee na yenye ladha ya aina yake itakuwa ni 
chaguo sahihi kwa wateja wanaopenda kuwa ‘wanaume wa kweli’ 
 “Ikiwa na kilevi cha asilimia 7.6% Alc, 
Plisner King, ambayo kauli mbiu yake ni ‘Kutana na Mfalme, kwa ajili ya Wanaume 
Imara na Wenye Ujasiri’, imetengenezwa kwa kuzingatia kanuni halisi za 
utengezaji wa bia ya kwanza ya Pilsner iliyotengenezwa huko Ulaya Mashariki,” 
anaeleza Mloka


Uzinduzi huo 
Ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, ambaye aliisifia kampuni 
ya SBL kwa kuonyesha njia katika ubunifu wa vinywaji vyenye kileo hapa nchini.


Mongela pia 
aliipongeza SBL kwa kufanya uwekezaji Mkoani Mwanza kupitia kiwanda chake cha 
bia ambacho amesema kimekuwa kikichangia maendeleo ya kiuchuni ya mkoa huo.


“Napenda 
kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wananchi wa  Mwanza kwa kampuni ya SBL. Uwekezaji wao hapa

Mwanza umesaidia upatikanaji wa  ajira za 
moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja pamoja na fursa za kibiashara kwa 
wakazi wa jiji hili,” alisema Mongela.


Pamoja na 
kiwanda cha Mwanza, SBL ina viwanda vingine viwili vya bia, kimoja kipo jijijni 
Dar es Salaam na kingine kipo Moshi mkoani Kilimanjaro. SBL inazalisha bia kama 
vile  Pilsner 
Lager, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness Stout and bia inayobeba 
bendera ya kampuni, Serengeti Premium ambayo imeshinda zaidi ya medali 10 za 
kitaifa na Kimataifa.

Related

Biashara 4421557003420964764

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item